Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Tovuti ya Kiebrania ya Walla! ikimnukuu mchambuzi wake wa masuala ya kijeshi, Amir Bohbot, imeripoti kuwa Islamic Revolutionary Guard Corps (IRGC) imefanya mabadiliko katika mifumo ya operesheni na kuimarisha uwezo wa makombora na ndege zisizo na rubani (drones), kwa kuzingatia tathmini za vita vya karibuni, ili kuongeza utayari kwa mzozo wowote wa baadaye.
Ripoti hiyo inadai kuwa kuongezeka kwa uzalishaji wa makombora ya mafuta imara, uendelezaji wa makombora ya balistiki na ya cruise, pamoja na upanuzi wa mifumo mbalimbali ya droni, kumeibua wasiwasi nchini United States na Israel kuhusu uwezekano wa Iran kutekeleza shambulio la kushtukiza.
Your Comment